Posts

Showing posts from August, 2019

Harry Maguire: Man Utd yamfanya beki wa Leicester kuwa ghali zaidi duniani

Image
Manchester United imemsaini beki wa kati a Uingereza Harry Maguire kutoka kwa wapinzani wao Leicester kwa dau la £80m - ikiwa ndio dau lililovunja rekodi ya beki ghali zaidi. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekubali kuweka kandarasi ya miaka 6 katika uwanja wa Old Trafford, huku akiwa na fursa ya kuongeza mwaka mmoja. Dau hilo la Maguire limepiku lile la £75m la Liverpool wakati walipomsaini beki Virgil van Dijk kutoka Southampton Januari 2018. ''Wakati Man United inapoanza kukulizia , ni fursa nzuri'', alisema Maguire Maguire ndiye mchezaji wa pili ghali zaidi kusainiwa katika ligi ya Uingereza baada ya Paul Pogba aliyejiunga na Man United kwa dau la (£89m), na anakuwa mchezaji wa pili ghali wa Uingereza aliye ghali baada ya winga wa Wales Gareth Bale, ambaye alijiunga na Real Madrid kutoka Tottenham kwa dau la £85m mwaka 2013. Ni mchezaji wa tatu kusajiliwa na mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer, baada ya Aaron wan Bisaka kuwasili kutoka Crystal Palace kwa...