Harry Maguire: Man Utd yamfanya beki wa Leicester kuwa ghali zaidi duniani

Manchester United imemsaini beki wa kati a Uingereza Harry Maguire kutoka kwa wapinzani wao Leicester kwa dau la £80m - ikiwa ndio dau lililovunja rekodi ya beki ghali zaidi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekubali kuweka kandarasi ya miaka 6 katika uwanja wa Old Trafford, huku akiwa na fursa ya kuongeza mwaka mmoja.
Dau hilo la Maguire limepiku lile la £75m la Liverpool wakati walipomsaini beki Virgil van Dijk kutoka Southampton Januari 2018.
''Wakati Man United inapoanza kukulizia , ni fursa nzuri'', alisema MaguireMaguire ndiye mchezaji wa pili ghali zaidi kusainiwa katika ligi ya Uingereza baada ya Paul Pogba aliyejiunga na Man United kwa dau la (£89m), na anakuwa mchezaji wa pili ghali wa Uingereza aliye ghali baada ya winga wa Wales Gareth Bale, ambaye alijiunga na Real Madrid kutoka Tottenham kwa dau la £85m mwaka 2013.
Ni mchezaji wa tatu kusajiliwa na mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer, baada ya Aaron wan Bisaka kuwasili kutoka Crystal Palace kwa dau la £50m huku naye winga Daniel James akijiunga na miamba hiyo kutoka Swansea kwa dau la £15m.
Maguire aliongezea: kufuatia mazungumzo yetu na mkufunzi, ninafurahia kuhusu maono na mipango aliyonayo kwa timu. Ni wazi kwamba Ole anajenga timu itakayoshinda mataji.
Kwa sasa nataraji kukutana na wachezaji wenzangu kabla ya msimu kuanza.
Solskjaer: Harry ni miongoni mwa wachezaji bora katika mchezo huu leo. Anajua kusoma mchezo na uwepo wake katika uwanja unaonekana huku akiwa na uwezo wa kutulia kunapotokea shinikizo.

Comments

Popular posts from this blog

DIVOCK ORIGI AZUNGUMZA KISWAHILI BAADA YA MECHI

TAARIFA MBAYA MASHABIKI WA MAN UNITED KUHUSU JUAN MATA

TOP TEN YA VILABU VYENYE THAMANI KUBWA DUNIANI