Posts

Showing posts from March, 2017

NYIMBO MPYA WIZKID FEAT DRAKE-COME CLOSER

Image
Audio mpya ya wizkid ambayo amemshirikisha drake in come closer hii nikutokana kusubiri muda mrefu mkali uyo wa dady yo kutoka nigeria ameachia ngoma kali akimusisha mkali wa hiphop drake kutoka marekani.     kwa audio download hapa  come closer     bofya hapa

FIFA IMEAMUA KUMLIPA MCHEZAJI ALIYEVUNJIKA MGUU KWENYE PAMBANO LA IRELAND VS WALES

Image
Baada ya usiku wa March 24 kuchezwa mchezo wa Jamhuri ya Ireland dhidi ya Wales na kumalizika kwa sare tasa ya 0-0, huku mchezo ukimalizika kwa masikitiko kutokana na staa wa Everton aliyekuwa anaichezea Ireland Seamus Coleman kuvunjika mguu kutokana na rafu aliyochezewa na Neil Taylor. Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA leo March 27 2017 limetangaza mambo mawili ikiwemo kumpa adhabu Neil Taylor lakini pia kuamua kumlipa mshahara Seamus Coleman kwa muda wote atakaokuwa nje ya uwanja wa akiuguza mguu wake.

UWANJA MPYA WA NDEGE WA KIMATAIFA MADEIRA WABADILISHWA JINA NA KUITWA RONALDO

Image
Moja kati ya vitu ambavyo vinaingia katika historia ya maisha ya staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid Cristiano Ronaldo ni uwanja wa ndege wa kimataifa wa Madeira kubadilishwa jina na kupewa jina lake

BRAZIL YAFUZU KOMBE LA DUNIA 2018 RUSSIA

Image
Brazil imekuwa timu ya kwanza kufuzu kombe la dunia bara la amerika kusini iyo ni baada ya kuifunga paraguay kwenye makundi kwa mabao 3-0

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA NA RAISI MAGUFULI IKULU DSM

Image
Waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn ameanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania, ambapo pamoja na mambo mengine mwenyeji wake rais Dk. John Magufuli, wanatarajia kutiliana saini mikataba kadhaa ya ushirikiano wa kiuchumi na biashara.

WAZIRI WA FEDHA WA AFRIKA KUSINI AFUKUZWA KAZI PRAVIN GORDHAN

Image
           Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amewafukuza kazi mawaziri wake kadhaa akiwemo Waziri wa fedha Pravin Gordhan pamoja na naibu wake Jonas Mkabisi ambao ndio waliokua sababu kuu ya kuwepo mabadiliko haya. Taarifa kutoka ikulu ya Afrika Kusini zinasema Malusi Gigaba ameteuliwa kuwa waziri mpya wa fedha.  Takriban mawaziri 15 wametimuliwa katika kile kinachotajwa kama mshangao kwa serikali ya Zuma Mapema wiki hii Gordhan aliamriwa kurudi nyumbani kutoka London alipokwenda kwa ziara ya kikazi, baada ya kutuhumiwa kuwa alikua akipanga njama za kuipindua serikali iliyopo madarakani. Maafisa kadhaa kutoka chama tawala cha ANC wanapinga kuondolewa kwa Gordhan

Mwili wa Kim Jong-un wawasili Korea Kaskazini

Image
Mwili wa Kim Jong-nam, ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, umewasili nchini Korea Kaskazini. Korea Kaskazini ilikuwa imeomba kupewa mwili huo lakini haikuwa imesema ulikuwa ni wa nani. Mwili huo ulitolewa kwa Korea Kaskazini kama sehemu ya makubaliano ambapo raia 9 wa Malaysia, waliizuiwa kuondoka Korea Kaskazini waliwasili nyumbani. Mwili wa Kim Jong-nam kusalimishwa kwa Korea Kaskazini Mzozo waibuka kati ya Korea Kaskazini na Malaysia Nchi hizo mbili zimekuwa kwenye mzozo wa kidiplomasia kufuatia mauaji ya Kim, kwenye uwanja wa Kuala Lumpur mwezi uliopita. Kila nchi ilikuwa imewapiga marufuku raia wa nchi nyingine kuondoka.  Raia watatu wa Korea Kaskazini wameruhusiwa kuondoka malaysia, kwa mujibu wa mkuu wa polisi wa nchi hiyo. Wanawake 2 kushtakiwa kwa mauaji ya Kim Jong nam Mshukiwa wa mauaji ya Kim Jong-nam alilipwa $90 Korea Kaskazini inashukiwa pakubwa kuhusika kwenye kifo cha bwana Kim, kwa kutumia kemikali ...

FIFA YAIDHINISHA KUWEPO KWA TIMU 48 KOMBE LA DUNIA.

Image
Kuwepo kwa timu 48 ilikua ni moja ya ahadi ya Gianni Infantino katika kampeni zake Chama cha soka duniani FIFA kimepanga kuwepo kwa michezo sita ili zipatikane timu zitakazoingia katika fainali za kombe la dunia mwaka 2020. FIFA imefafanua ni kwa namna gani timu 48 zitaweza kushiriki michuano hiyo. Rais wa shirikisho la soka Ulaya Aleksander Ceferin amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo na nchi za Ulaya zitawakilishwa vyema. Mchakato huo utakuwaje? Kila mwanachama wa FIFA atakuwa na uwezo wa kuongeza walau timu moja katika michuano ya mwaka 2026.    Mwenyeji wa fainali hizi ataingia moja kwa moja kama ilivyokua awali. Mapendekezo hayo yapo hivi Afrika - 9 kutoka timu za awali 5 Asia - 8 kutoka timu 4 za awali Ulaya - 16 kutoka timu 13 za awali Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean - 6 kutoka timu 4 za awali Bara la Oceania - 1 kutoka timu 1 ya awali Amerika ya Kaskazini - 6 kutoka timu 4 za awali Mwezi januari chama hicho che...