Kwa wapenzi wa Soka Afrika Mashariki jina la Divock Origi haliwezi kuwa geni kwao, huyu star wa soka anayeichezea Liverpool ya Uingereza lakini asili yake ni Kenya ambako pia baba yake mzazi aliwahi kuwa mchezaji maarufu. Baada ya kumalizika kwa game kati ya Liverpool na West Ham, Divock alizungumza na mtangazaji wa BBC Salim Kikeke na lugha iliyotumika kwenye mahojiano yao ilikuwa Kiswahili.
Kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea Man United ya England Juan Mata jina lake limerudi kwenye headlines baada ya kufanyiwa upasuaji wa groin, Mata ambaye mwanzoni mwa wiki hii alikuwa akilalamika mazoezini kuwa anasumbuliwa na groin amefanyiwa upasuaji. Taarifa zilizotoka usiku wa March 31 2017 kuhusu kiungo huyo ni kuwa upasuaji wake umeenda salama lakini kutokana na tatizo lake, kuna uwezekano mkubwa wa kukosa mechi zote za kumalizika za Man United tofauti na awali alivyotazamiwa kuwa anaweza kukosa mechi tatu tu.
Washindi wa Europa League msimu wa 2016/17 Manchester United ya England imetajwa kuwa Klabu yenye thamani zaidi 2017 ikizipiku miamba ya La Liga Real Madrid na Barcelona zilizokamata nafasi ya pili na tatu. kwa mujibu wa KPMG. Katika utafiti uliohusisha bei za matangazo, faida inayopatikana kwa mwaka, umaarufu, uwezo wa kimchezo na umiliki wa uwanja miongoni mwa klabu 32 za Ulaya, United imeibuka kinara kwenye list hiyo ikiwa na thamani ya euro 3.09b. Nafasi ya pili inakamatwa na mabingwa wa La Liga Real Madrid yenye thamani ya euro 2.97b huku Barcelona wakiwa katika nafasi ya tatu wakiwa na thamani ya euro 2.76 ambapo katika Top Ten England imeingiza klabu Sita ikifuatiwa na Uhispania yenye timu Mbili huku Ujerumani na Italia zikiwa na klabu moja moja kila nchi.
Comments
Post a Comment