EVERTON KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI TANZANIA
Klabu ya Uingereza ya Everton itazuru nchini Tanzania kwa mechi za kirafiki kabla ya msimu wa 2017/18.Kulingana na tovuti rasmi ya klabu hiyo, ziara hiyo ambayo ni ya kusheherekea udhamini mpya wa klabu hiyo na Sportpesa itakuwa na mechi ya kirafiki kati ya klabu hiyo na nyota wa Tanzania katika uwanja Taifa wa Dar es salaam wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 tarehe 13 Julai.
Everton itakuwa klabu ya kwanza ya ligi ya Uingereza kucheza katika taifa hilo la Afrika Mashariki, na itakabliana dhidi ya mshindi wa kombe hilo la Sportpesa.
- Simba sasa yadhaminiwa na SportPesa
- SportPesa watoa udhamini kwa Serengeti Boys
- Kenya kucheza dhidi ya Hull City Uingereza
Mchuano huo utashirikisha timu kutoka Tanzania na Kenya ambazo zitatoa timu nne kila moja wao.
Mapema mwezi huu Everton ilitangaza udhamini wa mamilioni ya pesa na Sportpesa ambapo jina la kampuni hiyo ya kamare litakuwa mbele ya tisheti za mabingwa hao wa Uingereza kwa miaka mitano.
Tangu kuanzishwa kwake nchini Kenya 2014 kampuni hiyo imedhamini vilabu vingi, kuwekeza mbali na kushiriki katika kamari.
Comments
Post a Comment