N’GOLO KANTE AMETWAA TUZO NYINGINE ENGLAND
Kiungo staa wa Ufaransa anayeichezea Klabu ya Chelsea ya England N’Golo Kante ametwaa tuzo nyingine msimu huu mara hii ikiwa ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Waandishi wa Habari za Michezo, FWA.
Katika hafla iliyofanyika Landmark Hotel Kante alipigiwa kura kushinda tuzo hiyo akiwapiku mchezaji mwenzie wa Chelsea Eden Hazard na mchezaji wa Tottenham Dele Alli kwa zaidi ya 65% ya kura zote.
Kabla ya tuzo ya FWA tayari N’Golo Kante alitwaa tuzo ya PFA na sasa anakuwa mchezaji wa 20 kutwaa tuzo hizo mbili kwa mkupuo mmoja.
Comments
Post a Comment