TAIFA STARS KUCHEZA NA MISRI


Kikosi cha wachezaji 20 wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania 'Taifa Stars' , kinatarajiwa kuondoka kesho Jumanne saa 10.45 jioni kwenda Misri.
Wachezaj hao wataungana na wengine watatu, naocheza soka la kulipwa ulaya ambao ni Nahodha Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Faridi Mussa kufanya jumla ya wachezaji kuwa 23 nchini Misri.
Nahodha Msaidizi, Jonas Mkude hatakuwako kwenye msafara huo kutokana na ushauri wa madaktari walioelekeza kwamba nyota huyo wa Simba apate mapumziko ya siku nne baada ya kupata ajali,
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga ameridhia na kusema kuwa Mkude ataungana na wenzake Juni 8, mwaka huu timu itakaporejea kutoka Misri. Mayanga hajajaza nafasi ya Mkude.
Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi 'L' kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Nchini Cameroon.

Comments

Popular posts from this blog

DIVOCK ORIGI AZUNGUMZA KISWAHILI BAADA YA MECHI

TAARIFA MBAYA MASHABIKI WA MAN UNITED KUHUSU JUAN MATA

TOP TEN YA VILABU VYENYE THAMANI KUBWA DUNIANI