WATANO WASHINDANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA LIGI KUU BARA



Wachezaji watano wameteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania kwa msimu wa 2016/2017.Walioteuliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho ni Aishi Manula (Azam FC), Haruna Niyonzima (Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Shiza Kichuya (Simba) na Simon Msuva (Yanga).
Majina hayo yatapigiwa kura na makocha, makocha wasaidizi na manahodha wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na wahariri wa michezo kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Wahusika watatumiwa fomu maalum za kupiga kura kwenye email za klabu zao na vyombo husika vya habari. Mwisho wa kupiga kura ni saa 6 usiku ya Jumanne, Mei 23 mwaka huu.
Hafla ya kutoa tuzo hiyo ambayo inaratibiwa na Kamati ya Ushauri ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika Mei 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

DIVOCK ORIGI AZUNGUMZA KISWAHILI BAADA YA MECHI

TAARIFA MBAYA MASHABIKI WA MAN UNITED KUHUSU JUAN MATA

TOP TEN YA VILABU VYENYE THAMANI KUBWA DUNIANI