WAYNE ROONEY AJIANDAA KURUDI EVERTON


Nahodha wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney anasema kuwa bado hajaamua kuhusu hatma yake katika klabu hiyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 hajachezeshwa sana msimu huu huku akiingia kama mchezaji wa ziada katika kombe la ligi ya Yuropa dhidi ya Ajax.
''Kuna maombi mengi mezani, Uingereza na ughaibuni'', alisema.
Rooney ambaye anaongoza kwa mabao 253 amesema kuwa angehamia Everton iwapo angesalia katika ligi ya Uingereza.
Inaaminika kwamba Rooney hataki swala la kandarasi yake mpya kuchukua muda mrefu hadi siku ya mwisho ya uhamisho mnamo tarehe 31 Agosti ,na ataondoka na familia yake kujadiliana na kuamua kuhusu hatua atakayochukua.
Rooney amesema kwamba hawezi kuichezea klabu nyengine yoyote katika ligi ya Uingereza isipokuwa Everton, huku meneja wa Toffees, Ronald Koeman na mkurugenzi wa soka Steve Walch wakisema wazi msimu huu kwamba wangemtaka mchezaji huyo iwapo atapatikana.
Rooney alijiunga na klabu hiyo ya Old Trafford kwa pauni milioni 27, 2004 na amefanikiwa kucheza takriban mechi 500 na kuvunja rekodi iliowekwa na Sir Bobby Charlton ya miaka 44 kwa kufunga mabao mengi msimu huu.

Comments

Popular posts from this blog

DIVOCK ORIGI AZUNGUMZA KISWAHILI BAADA YA MECHI

TAARIFA MBAYA MASHABIKI WA MAN UNITED KUHUSU JUAN MATA

TOP TEN YA VILABU VYENYE THAMANI KUBWA DUNIANI