RATIBA YA UFUNGUZI WA EPL 2017/2018
Klabu iliyopandishwa daraja majuzi Newcastle itakuwa mwenyeji wa Tottenham, nao Brighton wawakaribishe nyumbani Manchester City.
Wageni Huddersfield watazuru Crystal Palace.
Mechi ya kwanza ya Spurs katika uwanja wa Wembley itakuwa dhidi ya mabingwa wa Antonio Conte wikendi ya pili ya msimu.
Mechi za mwisho za ligi zitachezwa Jumapili 13 Mei, 2018 wiki moja mapema kuliko msimu uliopita kutokana na fainali za Kombe la Dunia ambazo zitaanza Urusi 14 Juni.
Ratiba ya mechi za Kombe la Ligi ya England itatolewa 21 Juni nayo ya mechi za Scotland siku mbili baadaye.
Mechi za ufunguzi Jumamosi, 12 Agosti, 2017
- Arsenal v Leicester City
- Brighton v Manchester City
- Chelsea v Burnley
- Crystal Palace v Huddersfield Town
- Everton v Stoke City
- Manchester United v West Ham United
- Newcastle United v Tottenham Hotspur
- Southampton v Swansea City
- Watford v Liverpool
- West Bromwich Albion v AFC Bournemouth
Spurs watatamba Wembley, na Arsenal je?
Kumekuwa na mashaka kuhusu uwezo wa Tottenham kutamba Wembley ikizingatia matokeo yao katika uwanja huo Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu uliopita.
Vijana hao wa Mauricio Pochettino watakuwa an kibarua kigumu mechi yao ya kwanza uwanja huo wao wa muda.
Mara ya mwisho walipokuwa Wembley, ilikuwa nusufainali Kombe la FA msimu uliopita ambapo walilazwa 4-2 na Chelsea.
Lakini wiki za kwanza huenda zikawa ngumu kwa mabingwa watetezi pia, huku Chelsea wakiwa wenyeji wa Everton (26 Agosti), wawatembelee washindi wa 2015-16 Leicester baada ya mapumziko ya kimataifa na kisha wawe wenyeji wa Arsenal (16 Septemba).
Vijana wa Arsene Wenger watakuwa an nafasi ya kuonyesha uwezo wao msimu ujao watakapozuru Anfield kucheza na Liverpool wiki ya tatu.
Mechi zitakazofuata Liverpool watazuru Etihad Stadium kukabiliana na Manchester City.
Katika hiyo, klabu zitacheza mechi nne katika kipindi cha siku sita wakati wa Krismasi na Mwaka Mpya, kwa jumla zitakuwa mechi nane kuanzia 2 Desemba hadi 1 Januari.
Wikendi ya pili na tatu
Jumamosi, 19 Agosti, 2017
- AFC Bournemouth v Watford
- Burnley v West Bromwich Albion
- Huddersfield Town v Newcastle United
- Leicester City v Brighton
- Liverpool v Crystal Palace
- Manchester City v Everton
- Stoke City v Arsenal
- Swansea City v Manchester United
- Tottenham Hotspur v Chelsea
- West Ham United v Southampton
Jumamosi, 26 Agosti, 2017
- AFC Bournemouth v Manchester City
- Chelsea v Everton
- Crystal Palace v Swansea City
- Huddersfield Town v Southampton
- Liverpool v Arsenal
- Manchester United v Leicester City
- Newcastle United v West Ham United
- Tottenham Hotspur v Burnley
- Watford v Brighton
- West Bromwich Albion v Stoke City
Comments
Post a Comment