TETESI ZA SOKA LEO BARANI ULAYA IJUMAA
Paris-Saint Germain wapo tayari kutoa kitita kitakachovunja rekodi ya dunia cha pauni milioni 119 kumsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco (Mirror).
Lakini Arsenal wanajiandaa kutoa dau jipya kumsajili Mbappe, huku Arsene Wenger akiwa na uhakika wa kumpata mchezaji huyo (Metro).
Mbappe hana tatizo la wazo la kwenda Emirates (Telegraph).
Dau la pauni milioni 100 kutoka Liverpool la kumtaka Kylian Mbappe limekataliwa (Marca).
Mbappe inasemekana amekuwa na mazungumzo na meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane (L'Equipe).
Meneja wa Chelsea Antonio Conte yuko tayari kumuuza kiungo Nemanja Matic, 28, kwenda Manchester United ili aweze kufanikisha usajili wa kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko, 22, kwa pauni milioni 42 (The Times).
Real Spciedad wamekubali kulipa pauni milioni 10 kumsajili winga wa Manchester United Adnan Januzaj, 22 (Daily Mail).
Beki Matteo Darmian wa Manchester United amempigia simu Jose Mourinho na kumuomba amsaidie katika kuhamia Juventus (Sun).
Mwenyekiti wa Stoke City Peter Coates amesisitiza kuwa hana mipango ya kumuuza Xherdan Shaqiri, 25, msimu huu (TalkSport).
Dau la pauni milioni 12 la Stoke kumtaka beki wa Middlesbrough Ben Gibson, 20, limekataliwa. Middlesbrough wanataka zaidi ya pauni milioni 20 (Mirror).
Tottenham wamewasiliana na Fiorentina, kumuulizia kiungo Matias Vecino, 25 (TalkSport).
Tottenham wapo tayari kutoa pauni milioni 17.5 kumsajili winga wa Schalke Max Meyer (Sun).
Spurs pia wanajiandaa kumpa mkataba mpya wa miaka mitano beki wa kulia Kieran Trippier, 26, (Mirror).
Liverpool wameambiwa na Borussia Dortmund kuwa mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang, 28, atagharimu pauni milioni 63 (Bild).
Liverpool wamekataa dau la pauni milioni 11 kutoka Napoli la kumtaka beki Alberto Moreno 24 (Telegraph).
John Terry anafikiria kwenda Aston Villa, huku akitarajia timu nyingine za Ligi Kuu zitamtaka pia (Guardian).
Antonio Conte amewaambia Chelsea kuwa anamtaka Leonardo Bonucci, 30, wa Juventus au Virgil van Dijk, 25 wa Southampton ili kuimarisha safu yake ya ulinzi (Guardian).
Burnley wana matumaini ya kuwakatisha tamaa West Brom katika mbio za kumsajili beki wa kushoto wa Leeds Charlie Taylor, 23 (Burnley Express).
Bayern Munich wapo tayari kumtoa kwa mkopo winga wa zamani wa Arsenal Serge Gnabry, baada ya kumsajili msimu huu, huku wakisaka jina kubwa katika ushambuliaji (SportBild).
Lyon wamekubaliana ada ya pauni milioni 16.7 kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Bertrand Traore, 21 (L"Equipe).
Intare Milan wanafikiria kupambana na Juventus katika kumsajili kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny, 28 (Evening Standard).
Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 100 wa Leonardo Bonucci na Alex Sandro kutoka Juventus
Manchester City wanazidi kuamini kuwa wataweza kumsajili Alexis Sanchez, 28, kwa pauni milioni 50. Chelsea nao wanataka kujaribu kupanda dau kumchukua Sanchez na watatoa dau rasmi hivi karibuni (Daily Mirror).
Arsenal wanataka kumfanya Jack Butland kuwa mrithi wa Petr Cech (Daily Star).
Comments
Post a Comment