TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMAPILI 02.9.2018
Meneja wa Manchester United
ameishauri klabu hiyo isimsaini mshambuliaji Cristiano Ronaldo msimu
ujao. Mchezaji huyo miaka 33 alihamia Juventus kutoka Real Madrid.
Sunday Mirror)
- Liverpool na Chelsea kileleni mwa jedwali la ligi EPL
Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 25, anasema anataka tena kujaribi kujiunga na Juventus mwezi Januari kutokana na kuendelea kudhoofika kwa uhusiano wake na Mourinho. (Tuttosport, via Manchester Evening News)
- Mourinho: Mimi ni bora duniani hata Man United isiposhinda ligi
Aliyekuwa mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 26, anawez kuhamia Arsenal au Chelsea ikiwa angeamua kuhamia Ligi ya Premia kwa sababu anapenda London. (Sunday Express)
- Mwanariadha wa Kenya ashinda mbio Ulaya licha ya kupoteza kiatu
Kiungo wa kati wa Spurs Eric Dier, 24, anatetea hatua ya klabu ya kutomsaini yeyote msimu ulioipita na kusema kuwa wana kikosi kizuri. (Mail on Sunday)
- Wachezaji 7 maarufu wanaotarajiwa kuhamia klabu mpya Ulaya
Kiungo wa kati wa West Ham Jack Wilshere hayuko katika kiwango cha kumwezesha kujumuishwa kwenye kikosi cha England na Southgate anasema mchezaji huyo wa miaka 26 ni lazima aanze kucheza vizuri ikiwa anataka kucheza mechi ya kimataifa. (Sunday Telegraph)
Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amekana kwamba amekosana na kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, lakini anasema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anahitaji kucheza maeneo tofauti katika klabu hiyo.. (Guardian)
Manchester United haijakiubaliana kuhusu mkataba mpya wa kumzuia mshambuliaji wake Anthony Martial ,22, kuondoka katika uwanja wa Old Trafford , huku raia huyo wa Ufaransa akiendelea na mazungumzo na klabu hiyo.(Goal)
West Brom ilifeli kumnunua kiungo wa kati wa Blackburn Rovers na Uingereza Bradley Dack, 24 kwa dau lililovunja rekodi la £15m. (Sun)
Comments
Post a Comment