TETESI ZA SOKA LEO BARANI ULAYA IJUMAA
Paris-Saint Germain wapo tayari kutoa kitita kitakachovunja rekodi ya dunia cha pauni milioni 119 kumsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco (Mirror). Lakini Arsenal wanajiandaa kutoa dau jipya kumsajili Mbappe, huku Arsene Wenger akiwa na uhakika wa kumpata mchezaji huyo (Metro). Mbappe hana tatizo la wazo la kwenda Emirates (Telegraph). Dau la pauni milioni 100 kutoka Liverpool la kumtaka Kylian Mbappe limekataliwa (Marca). Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 22.06.2017 Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 20.06.2017 Mbappe inasemekana amekuwa na mazungumzo na meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane (L'Equipe). Meneja wa Chelsea Antonio Conte yuko tayari kumuuza kiungo Nemanja Matic, 28, kwenda Manchester United ili aweze kufanikisha usajili wa kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko, 22, kwa pauni milioni 42 (The Times). Real Spciedad wamekubali kulipa pauni milioni 10 kumsajili winga wa Manchester United Adnan Januzaj, 22 (Daily Mail). Beki Matteo Darmian wa Manchester United am...