Posts

Harry Maguire: Man Utd yamfanya beki wa Leicester kuwa ghali zaidi duniani

Image
Manchester United imemsaini beki wa kati a Uingereza Harry Maguire kutoka kwa wapinzani wao Leicester kwa dau la £80m - ikiwa ndio dau lililovunja rekodi ya beki ghali zaidi. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekubali kuweka kandarasi ya miaka 6 katika uwanja wa Old Trafford, huku akiwa na fursa ya kuongeza mwaka mmoja. Dau hilo la Maguire limepiku lile la £75m la Liverpool wakati walipomsaini beki Virgil van Dijk kutoka Southampton Januari 2018. ''Wakati Man United inapoanza kukulizia , ni fursa nzuri'', alisema Maguire Maguire ndiye mchezaji wa pili ghali zaidi kusainiwa katika ligi ya Uingereza baada ya Paul Pogba aliyejiunga na Man United kwa dau la (£89m), na anakuwa mchezaji wa pili ghali wa Uingereza aliye ghali baada ya winga wa Wales Gareth Bale, ambaye alijiunga na Real Madrid kutoka Tottenham kwa dau la £85m mwaka 2013. Ni mchezaji wa tatu kusajiliwa na mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer, baada ya Aaron wan Bisaka kuwasili kutoka Crystal Palace kwa...

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMAPILI 02.9.2018

Image
Meneja wa Manchester United ameishauri klabu hiyo isimsaini mshambuliaji Cristiano Ronaldo msimu ujao. Mchezaji huyo miaka 33 alihamia Juventus kutoka Real Madrid. Sunday Mirror) Liverpool na Chelsea kileleni mwa jedwali la ligi EPL Mourinho anasema alijua kuwa msimu huu ungekuwa mgumu sana kwa Manchester United. (Daily Star Sunday) Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 25, anasema anataka tena kujaribi kujiunga na Juventus mwezi Januari kutokana na kuendelea kudhoofika kwa uhusiano wake na Mourinho. (Tuttosport, via Manchester Evening News) Mourinho: Mimi ni bora duniani hata Man United isiposhinda ligi Aliyekuwa nahodha wa Liverpool Graeme Souness anasema kiungo wa kati Pogba yuko tu kwenye klabu kuweza kudumisha thamania yake hadi United ipate kumuuza. (Sunday Times - subscription required) Aliyekuwa mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 26, anawez kuhamia Arsenal au Chelsea ikiwa angeamua kuhamia Ligi ya Premia kwa sababu anap...

TETESI ZA SOKA LEO BARANI ULAYA IJUMAA

Image
Paris-Saint Germain wapo tayari kutoa kitita kitakachovunja rekodi ya dunia cha pauni milioni 119 kumsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco (Mirror). Lakini Arsenal wanajiandaa kutoa dau jipya kumsajili Mbappe, huku Arsene Wenger akiwa na uhakika wa kumpata mchezaji huyo (Metro). Mbappe hana tatizo la wazo la kwenda Emirates (Telegraph). Dau la pauni milioni 100 kutoka Liverpool la kumtaka Kylian Mbappe limekataliwa (Marca). Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 22.06.2017 Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 20.06.2017 Mbappe inasemekana amekuwa na mazungumzo na meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane (L'Equipe). Meneja wa Chelsea Antonio Conte yuko tayari kumuuza kiungo Nemanja Matic, 28, kwenda Manchester United ili aweze kufanikisha usajili wa kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko, 22, kwa pauni milioni 42 (The Times). Real Spciedad wamekubali kulipa pauni milioni 10 kumsajili winga wa Manchester United Adnan Januzaj, 22 (Daily Mail). Beki Matteo Darmian wa Manchester United am...

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMANNE

Image
Chelsea wanajiandaa kuingia katika mbio za kutaka kumsajili Alex- Oxlade Chamberlain kutoka Arsenal, huku Liverpool na Manchester City wakimnyatia kiungo huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 23 (Mirror). Nemanja Matic, 28, anataka kwenda Manchester United kuungana na meneja wake wa zamani Jose Mourinho (Sun). Manchester City wanajiandaa kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre- Emerick Aubameyang, 28 (Sky Sports). Hata hivyo taarifa nyingine zinasema Manchester City hawana mpango wa kumsajili Pierre-Emerick Aubameyang (Express). Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 32, hatadai mshahara mkubwa ili kuhakikisha anaweza kuhamia Manchester United (Sun). Manchester United hawana uhakika kama wanataka kumsajili Ronaldo (Daily Express). Jose Mourinho amesema hataki kumsajili Ronaldo (Daily Star). Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ana wasiwasi kuwa huenda Cristiano Ronaldo anaitumia United ili kujipatia mkataba mpya Real ...

RATIBA YA UFUNGUZI WA EPL 2017/2018

Image
Klabu iliyopandishwa daraja majuzi Newcastle itakuwa mwenyeji wa Tottenham, nao Brighton wawakaribishe nyumbani Manchester City. Wageni Huddersfield watazuru Crystal Palace. Costa anaamini Chelsea hawamtaki Mechi ya kwanza ya Spurs katika uwanja wa Wembley itakuwa dhidi ya mabingwa wa Antonio Conte wikendi ya pili ya msimu. Mechi za mwisho za ligi zitachezwa Jumapili 13 Mei, 2018 wiki moja mapema kuliko msimu uliopita kutokana na fainali za Kombe la Dunia ambazo zitaanza Urusi 14 Juni. Ratiba ya mechi za Kombe la Ligi ya England itatolewa 21 Juni nayo ya mechi za Scotland siku mbili baadaye. Mechi za ufunguzi Jumamosi, 12 Agosti, 2017 Arsenal v Leicester City Brighton v Manchester City Chelsea v Burnley Crystal Palace v Huddersfield Town Everton v Stoke City Manchester United v West Ham United Newcastle United v Tottenham Hotspur Southampton v Swansea City Watford v Liverpool West Bromwich Albion v AFC Bournemouth Spurs watatamba Wembley, na Arsenal je?...

UEFA KUTOA TUZO TANO MWEZI AGOSTI

Image
Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) limetangaza kuanza kutolewa kwa tuzo tano mpya za wachezaji bora wa mwaka kuanzia Agosti hii ambazo washindi wake watapatikana toka kura za makocha na wanahabari. Tuzo hizo zitakabidhiwa huko Monaco nchini Ufaransa hapo Agosti 24 wakati wa droo ya makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya. Tuzo hizo 5 mpya ni kwa wachezaji waliofanya vyema kwenye mashindano ya klabu ya UEFA kwa msimu uliopita, kwa mwaka 2016/17,na zitatolewa sambamba na za mchezaji bora wa mwaka kwa wanaume na na wanawake.

REAL MADRID MABIGWA WAPYA WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2017

Image
Klabu ya Real Madrid ya Uhispania imeicharaza Juventus ya Italia 4-1 na kushinda Kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Mreno Cristiano Ronaldo alifunga mabao mawili, la kwanza kwake na klabu dakika ya 20 na lake la pili dakika ya 64 kutoka kwa krosi ya Luka Modric. Casemiro aliwafungia Real bao lao la pili dakika ya 61 kabla ya Marco Asensio kukamilisha ushindi wao dakika ya 90 kwa bao lao la nne. Juventus, waliokuwa wameanza vyema mechi hiyo wakikuwa wamekomboa bao la kwanza la Ronaldo dakika ya 27 kupitia Mario Mandzukic na kufanya mambo kuwa sare wakati wa mapumziko lakini kipindi cha pili mawimbi yaliwageuka. Nguvu mpya wao Juan Cuadrado alipewa kadi ya pili ya manjano dakika ya 84, baada ya kukaa uwanjani dakika 18 pekee. Gareth Bale aliingia kwenye mechi hiyo kama nguvu mpya dakika ya 77, mara yake ya kwanza kuchezeshwa mechi ya ushindani tangu 23 Aprili. Real Madrid wamefanikiwa kuwa klabu ya kwanza tangu AC Milan (1989, 1990) kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya...