Posts

Showing posts from May, 2017

KAHAMA COLLEGE OF HEALTH SCIENCES

Image
Mkuu wa chuo cha Afya Kahama anawatangazia nafasi za masomo kwa muhula wa septemba 2017/2018 kwa kozi zifuatazo:- 1. TECHNICIAN CERTIFICATE IN CLINICAL MEDICINE... MIAKA MIWILI. 2. DIPLOMA IN CLINICAL MEDICINE ………. MIAKA MITATU. 3. BASIC TECHNICIAN IN PHARMACEUTICAL SCIENCE..MWAKA MMOJA. 4. TECHICIAN CERTIFICATE IN PHARMACEUTICAL SCIENCES …… MIAKA MIWILI. 5. DIPLOMA IN PHARMACEUTICAL SCIENCES ………MIAKA MITATU. Kwa mawasiliano zaidi tutafute kwa namba hizi 0766640531, 0683170921.

TOP TEN YA VILABU VYENYE THAMANI KUBWA DUNIANI

Image
Washindi wa  Europa League  msimu wa 2016/17  Manchester United   ya  England  imetajwa kuwa Klabu yenye thamani zaidi 2017 ikizipiku miamba ya  La Liga  Real Madrid  na  Barcelona  zilizokamata nafasi ya pili na tatu. kwa mujibu wa  KPMG. Katika utafiti uliohusisha bei za matangazo, faida inayopatikana kwa mwaka, umaarufu, uwezo wa kimchezo na umiliki wa uwanja miongoni mwa klabu 32 za Ulaya, United imeibuka kinara kwenye list hiyo ikiwa na thamani ya  euro 3.09b. Nafasi ya pili inakamatwa na mabingwa wa  La Liga   Real Madrid  yenye thamani ya  euro 2.97b  huku  Barcelona   wakiwa katika nafasi ya tatu wakiwa na thamani ya  euro 2.76  ambapo katika  Top Ten  England  imeingiza klabu Sita ikifuatiwa na  Uhispania  yenye timu Mbili huku  Ujerumani  na  Italia  zikiwa na klabu moja moja kila nchi.

BARCELONA YAMTEUA KOCHA MWENGINE

Image
Barcelona wamemteua Ernesto Valverde kuwa mkufunzi wao mkuu kwa mkataba wa miaka miwili, ambapo anaweza akaongezewa mwaka mwingine wa tatu. Valverde ni mshambuliaji wa zamani wa Barca na alitangaza wiki iliyopita kwamba angeacha kazi Athletic Bilbao baada ya kuwaongoza kwa miaka minne. Anachukua nafasi ya Luis Enrique aliyetangaza Machi kwamba angeihama klabu hiyo iliyomaliza nafasi ya pili La Liga msimu huu. Anaondoka baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka mitatu. Pochettino asema hawezi kuwa mkufunzi Barca Messi aifungia Barcelona bao la 500 Enrique aliongoza Barcelona kushinda mataji matatu makuu msimu wake wa kwanza, mataji mawili makuu ya nyumbani mwaka 2016 na Kombe la Mfalme au Copa del Rey mwaka huu. Walilaza Alaves 3-1 mechi yake ya mwisho kuwa kwenye usukani katika fainali ya Kombe la Mfalme Jumapili. Rais wa Barca Josep Maria Bartomeu alimsifu Valverde, 53, kwa uwezo wake, ufahamu, ujuzi na busara na kusema: "Huwa anaendeleza wachezaji chipukizi na ...

MCHEZAJI GHALI ZAIDI DUNIANI AZURU MECCA

Image
Mchezaji soka aliye ghali zaidi duniani amefanya ziara ya kihujaji kwenda katika mji mkatatifu zaidi wa Kiislamu, Mecca, wakati wa mwanzo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba alipakia mtandaoni picha yake akiwa Mecca siku ya Jumapili na kuandika "kitu cha kupendeza zaidi nilichowahi kukitazama maishani mwangu." Aidha, aliandika ujumbe kwenye Twitter kutakia kila mtu "Ramadhani jema." Mourinho: Pogba apewe muda Mourinho: Pogba anaonewa'wivu' Pogba, 24, aliibuka mchezaji ghali zaidi katika historia majira ya joto mwaka jana, Manchester United walipowalipa Juventus ada ya £89m ($114m). Jumatano, alifunga bao na kusaidia Manchester United kulaza Ajax 2-0 na kushinda kombe la ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League mjini Stockholm, Sweden na pia kuwezesha klabu hiyo kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao. Baada ya kumalizika kwa msimu wa soka, Pogba alipakia mtandaoni video fupi yake na mkoba...

TAIFA STARS KUCHEZA NA MISRI

Image
Kikosi cha wachezaji 20 wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania 'Taifa Stars' , kinatarajiwa kuondoka kesho Jumanne saa 10.45 jioni kwenda Misri. Wachezaj hao wataungana na wengine watatu, naocheza soka la kulipwa ulaya ambao ni Nahodha Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Faridi Mussa kufanya jumla ya wachezaji kuwa 23 nchini Misri. Nahodha Msaidizi, Jonas Mkude hatakuwako kwenye msafara huo kutokana na ushauri wa madaktari walioelekeza kwamba nyota huyo wa Simba apate mapumziko ya siku nne baada ya kupata ajali, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga ameridhia na kusema kuwa Mkude ataungana na wenzake Juni 8, mwaka huu timu itakaporejea kutoka Misri. Mayanga hajajaza nafasi ya Mkude. Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi 'L' kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Nchini Cameroon.

FRANCESCO TOTTI AMWAGA MACHOZI AKIAGA AS ROMA

Image
Francesco Totti alitokwa na machozi alipokuwa anaaga baada ya kucheza mechi yake ya mwisho katika klabu ya AS Roma. Mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 40 amechezea klabu hiyo kwa miaka 25. Gianluigi Buffon kuchezea mechi ya ‘karne’ Katika kipindi hicho, amefunga mabao 307 katika mechi 786 alizocheza. Aliingia uwanjani mara ya mwisho dakika ya 54 mechi yao dhidi ya Genoa. Roma walishinda 3-2 kupitia bao la dakika ya mwisho la Diego Perotti ambalo liliwahakikishia nafasi ya kucheza hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Baada ya mechi, Totti alisoma barua kwa mashabiki, na kusema: "Naogopa. Sijui siku za usoni zitakuwaje." "Tafakari, kwamba wewe ni mtoto na umo katikati ya ndoto nzuri...na mamako anakuamsha uende shuleni. "Unajaribu kurejea kwenye ndoto yako...unajaribu sana lakini huwezi. "Wakati huu si kwamba ni ndoto, ni uhalisia. Na siwezi kurejea tena." Nahodha Totti pia alipewa nambari 10 iliyowekwa kwenye fremu, nambari ...

SIMBA KUJIPATIA TIKETI YA KOMBE LA CAF

Image
Baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu  Tanzania  bara msimu wa 2016/2017 wekundu wa Msimbazi  Simba  walisafiri hadi mjini  Dodoma  May 27 kucheza dhidi ya  Mbao FC  katika uwanja huru wa  Jamhuri Dodoma  kucheza mchezo wao wa fainali wa Kombe la  Azam Sports Federation Cup . Simba  waliingia katika mchezo huo wakiwa na jitihada za kuhakikisha wanapata ushindi na kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kutoshiriki kwa muda mrefu kutokana na kutopata nafasi ya Ubingwa wa Ligi Kuu au wa  FA . Katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na wabunge mbalimbali,  Simba  wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ya  Simba  yakifungwa na  Fredrick Blagnon  dakika ya 95 baada ya kupokea krosi nzuri kutoka kwa  Abdi Banda  na  Shiza Kichuya  dakika ya 120 aliyefunga kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa  Mbao  kushika Goli pekee la  Mbao FC ...

BERNADO SILVA ASAJILIWA NA MAN CITY KWA UERO 43M

Image
Manchester City wamekamilisha unuzi wa kiungo wa kati mshambuliaji wa Ureno Bernardo Silva kutoka kwa mabingwa wa ligi Ufaransa Monaco kwa £43m . Silva, 22, atajiunga na City mnamo 1 Julai. Mchezaji huyo ameichezea Monaco mechi 58 msimu huu, mbili dhidi ya City katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, na kufunga mabao 11 na kusaidia ufungaji wa mabao 12. Amechezea Ureno mechi 12 na kuwafungia bao moja. Vijana hao wa Pep Guardiola walimaliza Ligi ya Premia wakiwa nafasi ya tatu, na kujihakikishia nafasi ya kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao. Silva alisaidia Monaco kufika nusu fainali ya michuano hiyo msimu huu ambapo walishindwa na Juventus. Juventus watakutana na Real Madrid fainali Jumamosi tarehe 3 Juni.

EVERTON KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI TANZANIA

Image
Klabu ya Uingereza ya Everton itazuru nchini Tanzania kwa mechi za kirafiki kabla ya msimu wa 2017/18. Kulingana na tovuti rasmi ya klabu hiyo, ziara hiyo ambayo ni ya kusheherekea udhamini mpya wa klabu hiyo na Sportpesa itakuwa na mechi ya kirafiki kati ya klabu hiyo na nyota wa Tanzania katika uwanja Taifa wa Dar es salaam wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 tarehe 13 Julai. Everton itakuwa klabu ya kwanza ya ligi ya Uingereza kucheza katika taifa hilo la Afrika Mashariki, na itakabliana dhidi ya mshindi wa kombe hilo la Sportpesa. Simba sasa yadhaminiwa na SportPesa SportPesa watoa udhamini kwa Serengeti Boys Kenya kucheza dhidi ya Hull City Uingereza Mchuano huo utashirikisha timu kutoka Tanzania na Kenya ambazo zitatoa timu nne kila moja wao. Mapema mwezi huu Everton ilitangaza udhamini wa mamilioni ya pesa na Sportpesa ambapo jina la kampuni hiyo ya kamare litakuwa mbele ya tisheti za mabingwa hao wa Uingereza kwa miaka mitano. Tangu kuanzishwa kwake nchini...

WAYNE ROONEY AJIANDAA KURUDI EVERTON

Image
Nahodha wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney anasema kuwa bado hajaamua kuhusu hatma yake katika klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 hajachezeshwa sana msimu huu huku akiingia kama mchezaji wa ziada katika kombe la ligi ya Yuropa dhidi ya Ajax. ''Kuna maombi mengi mezani, Uingereza na ughaibuni'', alisema. Rooney ambaye anaongoza kwa mabao 253 amesema kuwa angehamia Everton iwapo angesalia katika ligi ya Uingereza. Inaaminika kwamba Rooney hataki swala la kandarasi yake mpya kuchukua muda mrefu hadi siku ya mwisho ya uhamisho mnamo tarehe 31 Agosti ,na ataondoka na familia yake kujadiliana na kuamua kuhusu hatua atakayochukua. Rooney amesema kwamba hawezi kuichezea klabu nyengine yoyote katika ligi ya Uingereza isipokuwa Everton, huku meneja wa Toffees, Ronald Koeman na mkurugenzi wa soka Steve Walch wakisema wazi msimu huu kwamba wangemtaka mchezaji huyo iwapo atapatikana. Rooney alijiunga na klabu hiyo ya Old Trafford kwa pauni mili...

REAL MADRID YAWEKA REKODI BAADA YA KUTWAA UBINGWA

Image
Mabao mawili ya  Cristiano Ronaldo  na  Karim Benzema  yaliiwezesha  Real Madrid  kutwaa taji la kwanza la  La Liga  tangu 2012 katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya  Malaga. Cristiano Ronaldo  alifunga bao la kuongoza dakika ya kwanza huku  Karim Benzema  akiongeza bao la pili baada ya mapumziko katika mchezo ambao  Real Madrid  walihitaji pointi moja tu kutwaa ubingwa Cristiano Ronaldo  ni mfungaji bora wa muda wote kwenye Ligi kuu tano za Ulaya (369), akimzidi  Jimmy Greaves  (366) Zinedine Zidane  anakuwa mchezaji wa zamani wa sita wa  Real Madrid  kushinda  La Liga  akiwa meneja, baada ya  Bernd Schuster,  Vicente del Bosque , Jorge Valdano,  Luis Molowny   na  Miguel Munoz

KOMBE LA DUNIA KULINDIMA JUNE MPAKA JULY 2018

Image
kombe la dunia litaanza kulindima june 15 mpaka july 15 uwanja wa moscow luzhniki ndo uwanja ambao utatumiwa kwa ufunguzinwa kombe la dunia na miji mingine itausishwa katika fainali za kombe la dunia miji ni kama  Kazan, Nizhny Novgorod, Sochi, Samara na robo fainali itafanyika st peterburg na nusu fainali itafanyika moscow.

DIVOCK ORIGI AZUNGUMZA KISWAHILI BAADA YA MECHI

Image
Kwa wapenzi wa Soka Afrika Mashariki jina la Divock Origi haliwezi kuwa geni kwao, huyu star wa soka anayeichezea Liverpool ya Uingereza lakini asili yake ni Kenya ambako pia baba yake mzazi aliwahi kuwa mchezaji maarufu. Baada ya kumalizika kwa game kati ya Liverpool na West Ham, Divock alizungumza na mtangazaji wa BBC Salim Kikeke na lugha iliyotumika kwenye mahojiano yao ilikuwa Kiswahili.

N’GOLO KANTE AMETWAA TUZO NYINGINE ENGLAND

Image
Kiungo staa wa Ufaransa anayeichezea Klabu ya  Chelsea   ya  England  N’Golo Kante  ametwaa tuzo nyingine msimu huu mara hii ikiwa ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Waandishi wa Habari za Michezo,  FWA. Katika hafla iliyofanyika  Landmark Hotel  Kante   alipigiwa kura kushinda tuzo hiyo akiwapiku mchezaji mwenzie wa  Chelsea  Eden Hazard  na mchezaji wa  Tottenham  Dele Alli  kwa zaidi ya  65%   ya kura zote. Kabla ya tuzo ya  FWA  tayari  N’Golo Kante  alitwaa tuzo ya  PFA  na sasa anakuwa mchezaji wa 20 kutwaa tuzo hizo mbili kwa mkupuo mmoja.

WATANO WASHINDANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA LIGI KUU BARA

Image
Wachezaji watano wameteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania kwa msimu wa 2016/2017.Walioteuliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho ni Aishi Manula (Azam FC), Haruna Niyonzima (Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Shiza Kichuya (Simba) na Simon Msuva (Yanga). Majina hayo yatapigiwa kura na makocha, makocha wasaidizi na manahodha wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na wahariri wa michezo kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini. Wahusika watatumiwa fomu maalum za kupiga kura kwenye email za klabu zao na vyombo husika vya habari. Mwisho wa kupiga kura ni saa 6 usiku ya Jumanne, Mei 23 mwaka huu. Hafla ya kutoa tuzo hiyo ambayo inaratibiwa na Kamati ya Ushauri ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika Mei 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

SERENGETI BOYS YATINGA UWANJANI KUPAMBANA ANGOLA LEO

Image
Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo inarejea Uwanja wa L'Amitie mjini Libreville kumenyana na Angola katika mchezo wake wa pili wa Kundi B Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17 zinazeondelea . Serengeti Boys inayofundishwa na Bakari Nyundo Shime, anayesaidiwa sana na Mshauri wa Ufundi, Mdenmark Kim Poulsen itahitaji ushindi katika mchezo wa leo kuweka hai matumaini ya kusonga mbele baada ya kulazimisha sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza na Mali, ambayo leo itamenyana na Niger.Kwa ujumla timu zote za Kundi B zitakuwa zinasaka ushindi wa kwanza leo, baada ya Angola pia kutoka sare ya 2-2 na Niger kwenye mchezo wa kwanza. Kundi A tayari Ghana imekuwa ya kwanza kutinga Nusu fainali baada ya kuwafunga wenyeji, Gabon mabao 5- 0 jana Uwanja wa Port Gentil.Mshambuliaji na Nahodha, Eric Ayiah aliye katika kiwango kizuri na kiungo, Emmanuel Toku kila mmoja alifunga mabao mawili leo, wakati Patmos Arhin aliyetokea benchi kipindi cha pili...